
Ukumbusho mdogo, baraka kubwa
Kiswahili · PDF · 32 pages · Updated October 2026
TZS 1,500
Kitabu hiki ni mwongozo wa kila siku kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kikiwa na hadithi sahihi zilizopangwa kwa siku 30. Kila ukurasa unakuletea ukumbusho wa kiroho, mafunzo ya kivitendo, na tafsiri kwa Kiswahili na Kiingereza ili msomaji apate manufaa kwa urahisi.
🌙 Ndani ya kitabu hiki utapata:
Hadith sahihi kuhusu kufunga, kuswali, na kujenga taqwa.
Ukumbusho wa kila siku unaoimarisha imani na maadili.
Tafsiri sambamba kwa Kiswahili na Kiingereza kwa urahisi wa kujifunza na kufundisha.
Mafunzo yanayounganisha ibada na maisha ya kila siku.
✨ Kwa nini kitabu hiki ni muhimu:
Ramadhani ni mwezi wa rehema, msamaha na baraka. Ukumbusho wa Kila Siku Ramadhani ni rafiki wa kila muumini anayetaka kuishi Ramadhani kwa uelewa, nidhamu na ukaribu zaidi na Allah. Ni chaguo bora kwa wanafunzi, walimu, familia na waumini wote wanaotafuta mwongozo wa kila siku.
"Ukumbusho mdogo, baraka kubwa"

Guidance Cordinator
Kama nyuki anayezunguka takribani maua 3000-4,000 ili kutengeneza mililita moja ya asali ambayo mnywaji anaweza kunywa mara moja na kuimaliza, vivyo hivyo waandishi huzunguka vyanzo vingi vya maarifa na tafsiri wakikusanya vipande vidogo vya hekima na kuviunganisha kwa juhudi kubwa, na msomaji hunufaika kwa kitabu kimoja ambacho anaweza kukisoma na kukimaliza mara moja; hivyo, mfano huu unatosha kuwa motisha kwa wenye akili, na unafupisha kwa uwazi faida ya kusoma na kunufaika kutoka kwenye vitabu. Khalifa Loishorwaki Simion alizaliwa Arusha, Tanzania, na kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Cairo, Misri (mwaka 2020) – moja ya vyuo vikongwe na vyenye heshima kubwa zaidi duniani katika masomo ya dini ya Kiislamu. Elimu hii imemjengea msingi imara wa kuchambua na kufundisha masuala ya kidini kwa umahiri na uaminifu.
Visit Sheikh Khalifa L. Simion's shop →